Ofisi ya Rais DRC yajiunga na uchunguzi wa mauaji ya balozi wa Italia

-

Maafisa kutoka ofisi ya rai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanatarajiwa kupelekwa mjini Goma kusaidia katika uchunguzi wa mauaji ya balozi wa Italia nchini humo.

Maafisa hao wataondoka leo kuelekea Goma na watakuwa wakiwasilisha ripoti kwa za mara kwa mara kwa rais.

- Advertisement -

“Mjumbe wa rais wa DRC atazuru [Italia] Jumanne ya leo Februari 23 kuwasilisha barua ya kibinafsi kwa rais wa baraza la Italia,” Kulingana na ripoti kutoka kwa idara ya Idara ya habari ya rais.

Katika ujumbe uliyochapishwa katika mtandao wa Twitter, Rais Félix Tshisekedi alisema alisikitishwana taarifa za kufuatia kuuawa kwa mwanadiplomasia wa Italia, Luca Attanasio.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you