Serikali yaandaa ndege mbili za kuangamiza nzige

-

 

Serikali imesema katika kukabiliana na makundi ya nzige waliovamia maeneo mbalimbali ya wilayani Longido wakitokea nchi jirani ya Kenya itatumia ndege maalumu za kupulizia dawa ili kuwaangamiza kabla hawajasababisha hasara.

- Advertisement -

Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema tayari serikali imeshaanza kuchukua hatua na ndege ya shirika la chakula ulimwenguni (FAO) kutoka Nairobi,Kenya itaanza kuwaangamiza nzige hao kuanzia Februari 22, 2021 (kesho Jumatatu).

“Jitihada zinaendelea kuchukuliwa na Wizara ya Kilimo ili kuwadhibiti wasilete madhara zaidi,  Waziri wa Kilimo,Profesa Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wake,Gelard Kusaya wapo wilayani Longido kujionea hali ilivyo kwa ajili ya kuchukua hatua zinazopaswa,”amesema Mwaisumbe.

Amesema ndege ya pili ambayo ni mali ya serikali itaanza kazi ya kuwaangamiza nzige hao mara baada ya rubani kurejea nchini kutoka Ethiopia alikoombwa kufanya kazi ya kupulizia dawa kwa kutumia ndege maalumu.

Taarifa za kuingia makundi ya nzige nchini zilipatikana juzi Ijumaa ambazo zilithibitishwa na Mwaisumbe mwenyewe alipohojiwa na vyombo vya habari.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you