Steinmeier aonya dhidi ya kuongezeka chuki dhidi ya Wayahudi

-

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameusifu mchango wa Wayahudi kwa utamaduni wa Wajerumani na kusema kuwa historia yao katika nchi hiyo ni “ya ukombozi na ustawi, lakini pia ya udhalilishaji, kutengwa na kunyimwa haki.

” Akizungumza katika sinagogi moja la mjini Cologne, kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 1,700 ya maisha ya Kiyahudi nchini Ujerumani, Steinmeier alisema iwe ni katika filosofia, fasihi, uchoraji, muziki, sayansi, au biashara, Wayahudi wamesaidia kuijenga historia ya Ujerumani na kuufanya utamaduni wa nchi hiyo kuangaza. 

- Advertisement -

Rais Steinmeier hata hivyo alikiri kuwa maisha ya Kiyahudi yanatishiwa kutokana na hisia za wazi za kupinga Uyahudi akihimiza kuwa ni muhimu kupambana na wimbi hilo. 

Rais wa Baraza Kuu la Wayahudi Josef Schuster alisema Wayahudi hawatasherehekea mwaka huu kutokana na mashambulizi ya karibuni kwenye taasisi za Kiyahudi na ongezeko la chuki dhidi ya Wayahudi. 

Rais wa Israel Reuven Rivlin alisisitiza urafiki wa kina kati ya Ujerumani na Israel, akisema kuwa ijapokuwa hawatosahau majanga ya zamani, nchi zote zina urithi wa pamoja.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you