Kwa mara ya kwanza Donald TRump atatoa hotuba baada ya kuachia wadhifa wake kama Rais wa Marekani.
Kulingana na Tovuti ya habari ya ‘The Hill’, ambayo inafuatilia kwa karibu siasa za Marekani,
“Trump atazungumza kwenye jukwaa la umma kwa mara ya kwanza tangu aondoke Ikulu.”.
Inasemekana kwamba Donald Trump atazungumza katika mkutano wa kila mwaka wa Chama cha kisiasa cha CPAC huko Orlando, Florida, mwezi huu, huku tarehe rasmi ya mkutano huo ikiwa haijabainishwa
Imebainika kuwa Trump, ambaye atatokea mbele ya kamera kwa mara ya kwanza ndani ya wiki, anatarajiwa kuzungumzia sera za Chama cha Demeocrat na mustakabali wake.
Imesisitizwa kuwa Trump, ambaye amepanga kuzungumza katika mkutano huo atalenga sera za mipaka za Rais wa sasa Joe Biden.