Uingereza kuondoa lockdown leo

-

Waziri Mkuu Boris Johnson anatarajiwa kuanza kuondoa amri ya tatu– na ikiwezekana– ya mwisho ya kudhibiti matembezi na mikusanyiko kutokana na virusi vya corona, wakati kasi ya kuchanja wananchi ikiweka ahueni kwa hospitali ambazo ziliathirika vibaya.

- Advertisement -

Katika taarifa yake kwa bunge, Johnson anatarajiw akuthibitisha kufunguliwa kwa shule zote Machi 8 katika hatua ya kwanza kubwa kuirudisha nchi katika hali ya kawaida, ikiwa ni karimu mwaka mmoja tangu alipotoa amri ya kutaka wananchi wasitoke majumbani.

Waziri huyo mkuu mhafidhina ambaye alituhumiwa kuchelewa kufanya maamuzi na kuwahi kulegeza masharti mwaka jana, anasema ataweka mpango ambao utahakikisha nchi hairudi katika lockdown.

“Leo nitaweka mpango ambao utatuondoa kwa makini katika lockdown,” alisema katika taarifa yake kabla ya kwenda Bunge la Makabwela na baadaye kufanya mkutano na waandishi wa habari.

“Mara zote kipaumbele chetu kimekuwa na kurejesha watoto shuleni ambacho tunajua ni muhimu kwa ajili ya elimu yao sambamba na akili na miili yao, na pia tutaweka umuhimu kwa watu kuungana tena na wapendwa wao kwa usalama.”

Uingereza ni moja ya nchi zilizoathiriwa sana na ugonjwa wa virusi vya corona, ikiwa na vifo zaidi ya 120,000.

Ilikuwa nchi ya kwanza kuanza kuchanja wananchi mwezi Desemba, lakini kukua kwa maambukizi kulisababisha irejee katika amri ya kudhibiti watu kutembea na mikusanyiko.

Zaidi ya watu milioni 17 sasa wameshachanjwa angalau dozi ya kwanza, idadi hiyo ikiw ani theluthi moja ya Waingereza.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you