Umoja wa Ulaya kuidhinisha vikwazo dhidi ya Urusi

-

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya kesho wanatarajiwa kutoa ridhaa ya kuikewa vikwazo Urusi kwa kumfunga mkosoaji wa serikali ya nchi hiyo Alexei Navalny na kuwakandamiza waandamanaji. 

- Advertisement -

Wanadiplomasia hao wa ngazi ya juu kutoka mataifa 27 wanachama wa umoja huo watakutana mjini Brussels kwa mazungumzo ambayo pia yatajumuisha majadiliano na Waziri Mpya wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. 

Serikali za kanda hiyo pia zinalenga kutumia masharti mapya ya Umoja wa Ulaya kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu kuwawekea vikwazo wote wanaohusika na ukandamizaji nchini Urusi ikiwemo kuzuia mali na kuwanyima visa ya kuingia Ulaya. 

Umoja wa Ulaya tayari ulikwishaiweka Urusi vikwazo vingine tangu nchi hiyo ilipolinyakua eneo la Crimea mwaka 2014 na kuchochea vita nchini Ukraine.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you