Viongozi wa jeshi la Myanmar wameongeza muda wa kumzuia Suu Kyi

-

 

Viongozi wa jeshi la Myanmar wameongeza muda wa kumzuia kiongozi aliyeondolewa madarakani Aung San Suu Kyi, muda ambao ulitarajiwa kukamilika jana Jumatatu.

Watu wameandamana nchini humo kupinga mapinduzi ya kijeshi na kurejesha utawala wa kiraia na pia wanashinikiza kiongozi huyo kuachiliwa huru

- Advertisement -

Kwa mujibu wa wakili anayemuwakilisha Suu Kyi, Khin Maung Zaw, kiongozi huyo atazuiliwa rumande hadi Februari 17 wakati ambapo huenda akafikishwa kortini na vikao hivyo kuendeshwa kwa njia ya video.

Aung Suu Kyi ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel yuko chini ya kizuizi cha nyumbani kwa shtaka la kuingiza nchini humo redio sita za upepo kinyume cha sheriaKuendelea kuzuiliwa kwa Suu Kyi huenda kukazidisha mivutano zaidi kati ya waandamanaji na jeshi, ambalo lilichukua madaraka kupitia mapinduzi mnamo Februari 1.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you