Afrika Kusini kuanza kutoa vyeti vya chanjo ya COVID-19

0
1

“ Wizara ya Afya hivi karibuni itaanza kutoa cheti cha chanjo cha COVID-19 ambacho kitaonyesha uthibitisho rasmi wa chanjo.

Cheti hicho kitatumika kuwezesha safari na mikusanyiko na shughuli nyingine ambazo zinahitaji uthibitisho wa chanjo,” ameeleza.

Ramaphosa pia amelegeza masharti ya ndani dhidi ya janga la corona, ikiwemo kupunguza muda wa masharti ya kutoka nje, ameondoa marufuku ya uuzaji wa pombe majira ya usiku, na kuruhusu mikusanyiko mikubwa.

Amesema serikali ina mpango wa kutoa dozi za chanjo 250,000 kila siku hadi katikati ya mwezi Desemba.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP