Kiongozi wa Algeria ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo hii, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa taifa hilo, Abdelaziz Bouteflika, ambaye utawala wake miaka 20, unatajwa kugubikwa na rushwa na aliondoshwa madarakani kwa maandamano makubwa baada ya kutaka kugombea madaraka kwa muhula mpya.

Bouteflika aliyefikwa na maradhi ya kiharusi mwaka 2013, alifariki dunia Ijumaa, akiwa na umri wa miaka 84. 

Katika siku zake za mwisho za urais wake alikuwa akionekana kwa nadra sana.Rais huyo zamani hajaonekana kabisa hadharani tangu, Rais Abdelmadjid Tebboune achukuie hatamu ya uongozi wa Algeria. 

Ofisi ya rais huyo wa sasa imesema katika maombolezo hayo ya siku 3 bendera zitapepea kwa nusu mlingoti.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles