Algeria imefunga anga zake kwa anga zote za kiraia na za kijeshi za Morocco, urais wa Algeria umesema.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya mkutano wa Baraza Kuu la Usalama linaloongozwa na Rais Abdelmadjid Tebboune.

Hatua hii inajiri “kwa sababu ya uchochezi unaoendelea na vitendo vya uhasama kwa upande wa Morocco”, ilisema katika taarifa.

Algiers iliilaumu Rabat kwa kuunga mkono MAK,kundi lililojitenga ambalo serikali liliitambua kama shrikala la kigaidi.

Morocco haijatoa tamko rasmi kuhusiana na uamuzi huo. Chanzo cha Habari katika shirika la Habari la Royal Air Maroc kimenukuliwa na Reuters kikisema kuwa ufungaji huo wa anga utaathiri ndege 15 kila wiki ambazo zinahudumu kati ya Morocco, Tunisia,Uturuki na Misri.

Mamlaka zinalaumu kundi hilo kwa kuhusika na moto mkali wa porini, haswa huko Kabylie, ambao uliua watu wasiopungua 65. MAK imekanusha madai hayo.

Ikijibu hatua hiyo Morocco ilisema kuwa Algeria haina msingi wa kukatiza uhusiano kati yao ikiongeza kuwa madai yao ni ya “uwongo na ya kujinga.”

Mpaka kati ya Morocco na Algeria umefungwa tangu mwaka 1994 na Algeria imeashiria kuwa itabadilisha usafirishaji wa gesi kutoka kwa bomba inayopita Morocco, hatua ambayo inatarajiwa kutekelezwa upya baadaye mwaka huu.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles