Lemi Luchumi mwenye ulemavu wa ngozi, ambaye alikuwa mkazi wa Mamba, Mlele mkoani Katavi na kuhama kijijini hapo baada ya kukatwa mkono na watu wasiojulikana mwaka 2015, anahofia kurudi kijijini hapo kwamba huenda watu hao wakammalizia na kuiomba serikali imsaidie kusomesha wa watoto wake.

Akizungumza na EATV amesema baada ya kupoteza mkono wake serikali ilimuondoa kijijni hapo kwa ajili ya usalama wake lakini baada ya muda alipaswa kurejea nyumbani ila kutokana na hali ya mazingira ya kijiji hicho bado anahofu na imemlazimu kuishi mji mdogo wa kibiashara wa Majimoto huku akikabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Akiendelea kutoa simulizi, Lemi  amesema ana jumla ya watoto watano lakini kutokana na kukosa pesa ya kuwanunulia mahitaji muhimu ya shule watoto wake na kwa sasa amepoteza uwezo wa kufanya kazi kama ilivyokuwa hapo awali.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles