More
  - Advertisement -

  Amnesty International: Janga la covid linatumiwa kubinya haki

  -

  - Ad Keep reading below -

  Ripoti ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International iliotolewa leo inaelezea kuhusu madhila ya janga la Covid-19 kwa walio wachache, wahudumu wa afya na wanawake katika nchi kadhaa duniani.

  Ripoti ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International iliotolewa leo inaelezea kuhusu madhila ya janga la Covid-19 kwa walio wachache, wahudumu wa afya na wanawake katika nchi kadhaa duniani. Ripoti hiyo inaelezea kwamba janga la Covid-19 linatumiwa na viongozi katika kubinya haki za binadamu. Mkuu mpya wa shirika hilo Agnes Callamard, ametoa mwito kwa ajili ya kurekebishwa kwa mifumo kadhaa iliochakaa,ukiwemo mfumo wa afya. 

  - Ad Keep reading below -

   Ripoti hiyo ya mwaka 2020 na 2021 ya shirika la Amnesty International inaangazia haki za binadamu katika nchi 149 kote duniani. Kwenye ripoti hiyo, shirika la Amnesty linasema kuwa raia ambao tayari walikuwa wameathirika na kutengwa na uongozi wakiwemo wanawake na wakimbizi ndio walioathirika sana na janga hili la Covid-19.

  ALSO READ  Watu zaidi ya 40 wamefariki kutokana na mafuriko Korea Kusini
  ALSO READ  Somalia Continues Offensive Against Kenya

   Wahudumu wa afya,wafanyakazi wahamiaji na watu wanaofanya kazi kwenye sekta ya biashara rejareja na ambao wengi wao walikuwa kwenye mustari wa mbele katika kupambana na corona,walifadhahishwa pia na mfumo wa afya uliochakaa na misaada ya kiutu ya kusuasua.

  - Ad Keep reading below -

  Hatua za vizuwizi zilizochukuliwa na baadhi ya viongozi zilichangia pia kubinya haki za binadamu,linaelezea shirika la Amnesty International.

  Agnes Callamard, mkuu mpya wa shirika la Amnesty International amesema kuwa janga la Covid-19 liliongeza tofauti na kuvuruga huduma za idara za umma.

  Ripoti hiyo inaonyesha pia mpasuko wa miongo kadhaa ya uongozi mbaya dhidi ya waliowachache,wakimbizi, wazee na wanawake katika kipindi cha janga la Covid-19.

  Shirika la Amnesty International, limetoa mfano wa Uganda ,nchi ambayo inawapokea wakimbizi milioni 1.4, ilifunga mipaka yake mara lilipozuka janga la Corona bila kutofautisha wakimbizi na watu wanao omba hifadhi waliotaka kuingia nchini humo. Kinyume cha hatua hiyo ni kwamba zaidi ya watu elfu kumi walizuwiliwa kwenye mpaka baina ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

  ALSO READ  DCI Boss Given Public Beating
  - Ad Keep reading below -

  Nchini Tanzania, serikali ili bana vyombo vya habari,ikielezea kwamba vinasambaza uvumi kuhusu janga la Covid-19, huku mwezi Juni, aliekuwa rais wake John Magufuli akitangaza kuwa Tanzania haina corona. Vyombo vya habari vilifungwa kwa sababu ya kutangaza taarifa za upinzani.

  ALSO READ  Wakurugenzi wakutana kuboresha mwongozo wa ukopaji na upokeaji misaada

  Polisi nchini Kenya,walitumia nguvu ya kuzidi kiasi,iliyosababisha hadi mauwaji, kwa ajili ya kuheshimisha hatua ya vizuwizi vilivyo wekwa.

   Kupigwa,kutoweka na kamatakamata ya wapinzani ama wafuasi wao vilishuhudiwa pia nchini Burundi na shirika la Amnesty International mnamo kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

  Nchini Rwanda, shirika la Amsety International linasema visa vya kesi zisizo za haki na huru,kukamtwa kinyume cha sheria na matumizi ya nguvu ya kupindukia kiasi viliendelea nchini humo.

  Na huko Nchini Congo, mauwaji ya raia yanaendelea kwenye majimbo ya Kivu, huku wanaharakati wa haki za binadamu wakitishiwa maisha yao. Inaelezea ripoti hiyo ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.

   

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Oduduwa Republic: Tell us your plans for Yoruba Muslims – Islamic group tells agitators

  The Ooni of Ife, Adeyeye Enitan Ogunwusi Ojaja II, has appealed to Nigeria’s Ambassador Designate to Jamaica, Belize, Haiti and Dominican Republic, Dr. Maureen...

  Paraguay’s ‘Life and Death’ Covid Crisis Gives China Diplomatic Opening

  RIO DE JANEIRO — Taiwan has built thousands of homes for the poor in Paraguay, upgraded the country’s health care system, awarded hundreds...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -