Shirika la kutetea haki la Amnesty International limemtuhumu Rais wa Gambia Adama Barrow

ya kushindwa kufuta sheria kandamizi zinazodhibiti uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Shirika hilo linasema limesema nchi hiyo imeredi zaidi ya mashambulio 15 kwa waandishi wa habari katika miaka minne iliyopita, kulingana na ripoti yake iliyotolewa Jumatano.

Rais Barrow aliingia madarakani mnamo 2017 kwa ahadi ya kampeni ya kurekebisha makosa ya mtangulizi wake, Yahya Jammeh.

Lakini Amnesty inasema sheria hzi kandamizi zinazodhibiti haki za binadamu, pamoja na uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani hazijarekebishwa.

Baadhi ya taasisi za serikali pamoja na vyombo vya usalama vya kitaifa vinaweza kufuatilia, kukatiza na kuhifadhi mawasiliano kwa madhumuni ya ufuatiliaji bila amri ya mahakama.

Katika uamuzi wa mwaka 2018, Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS iliamuru mamlaka za Gambia kufanyia marekebisho sheria ya kashfa, fitna na habari za uwongo kulingana na majukumu ya nchi hiyo chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Hilo halijafanyika kwa sababu bunge la sasa linaelekea kumaliza kipindi chake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles