Swahili News

Aweso ataja vipaumbele bajeti ya 2022/23

By Sharon Sauwa

Dodoma. Wizara ya Maji imeliomba Bunge kuwaidhinishia Sh709.36 bilioni katika mwaka wa fedha 2022/2023 huku ikitaja vipaumbele saba vya bajeti hiyo ikiwemo ujenzi wa miradi mipya katika miji 28 nchini.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameomba fedha hizo leo Alhamis Mei 12, 2022 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2022/2023.

Amesema kati ya fedha hizo, matumizi ya kawaida ni Sh51.46 bilioni ambapo Sh16.7 bilioni sawa na asilimia 32.45 ni kwa ajili ya kugharamia matumizi mengineyo.

Amesema Sh34.7 bilioni sawa na asilimia 67.55 ni kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wa wizara, Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) na Chuo cha Maji.

JOIN US ON TELEGRAM

Aweso amesema bajeti ya maendeleo ni Sh657.89 bilioni ambapo kati ya fedha hizo, Sh407.06 bilioni sawa na asilimia 61.87 ni fedha za ndani na Sh250.83 bilioni sawa na asilimia 38.13 ni fedha za nje.

Waziri huyo ametaja vipaumbele vya wizara hiyo kuwa ni kukamilisha ujenzi, ukarabati na upanuzi wa miradi inayoendelea kutekelezwa na kuanza ujenzi wa mabwawa ya kimkakati ya Kidunda na Farkwa.

Vingine ni kuanza ujenzi wa miradi ya maji mipya ikiwemo miradi ya maji katika miji 28, kuendelea na utunzaji wa vyanzo vya maji ikihusisha kutambua na kuweka mipaka na kutangaza kwenye gazeti la Serikali ili vyanzo hivyo vilindwe kisheria.

Aweso ametaja kipaumbele kingine ni kutekeleza miradi ya maji kwa kutumia vyanzo vya uhakika ikiwemo maziwa makuu na mito mikubwa.

This article Belongs to
News Source link

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button
Muhabarishaji News We would like to show you notifications for the latest news and updates.
Dismiss
Allow Notifications

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker