AfricaSwahili News

Azam FC yaizidi kete Simba, Manyama atua Azam

Beki wa timu ya Taifa ya Tanzania,  Edward Manyama ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Ruvu Shooting sasa ni mali ya Azam FC. 

Beki huyo awali alikuwa anatajwa kumalizana na Simba kwa dili la miaka miwili sasa Azam FC wamepindua meza na kumpa dili la miaka mitatu. 

Huu unakuwa ni usajili mkubwa wa kwanza kwa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina  kwa mchezaji mpya mbali na wale ambao wameongezewa kandarasi zao ikiwa ni pamoja na David Bryson. 

 

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button