AfricaSwahili News

Balozi Mulamula amuaga Balozi wa India

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amemuaga Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini.

Akiongea katika hafla ya kumuaga balozi wa India iliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Waziri Mulamula amempongeza Balozi Kohli kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya India na Tanzania.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula amemuahidi Balozi Kohli kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na India katika sekta za elimu, afya, maji, kilimo, tehama na utalii kwa maslahi mapana ya nchi zote mbili.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nakuahidi ushirikiano kutoka kwetu, nakutakia kila la kheri katika maisha yako nje ya Tanzania na ni imani yangu kuwa utakuwa balozi mzuri wa Tanzania duniani,” Amesema Balozi Mulamula

Kwa upande wake Balozi Kohli ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.

Balozi Kohli ameelezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya India na Tanzania na amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha diplomasia ya uchumi.

 

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.