Mwimbaji Staa wa Bongofleva Ben Pol amefungua shauri la talaka Mahakamani dhidi ya Mke wake Anerlisa ambae ni Raia wa Kenya ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kilichoongea na millardayo.com shauri hilo limefunguliwa na Benard Paul Mnyang’anga katika Mahakama moja ya Mwanzo Jijini Dar es salaam, hata hivyo bado haijafahamika sababu za Mwimbaji huyu kuamua kuivunja ndoa hiyo.
Ben Pol na Anerlisa walifunga ndoa mwishoni mwa mwezi May mwaka 2020 katika Kanisa Katoliki la St. Gaspar Mbezi Beach, Dar es salaam na kuhudhuriwa na Watu wachache kutoka upande wa familia zote mbili pamoja na Marafiki wachache wa karibu wa familia.
Hamna mtu anaependa kuwa Single. Kuwa single sio kwamba mtu hujui kupenda. Sababu kubwa ni kuchoka kujitoa kwa mtu halafu mwishoni unapata maumivu.
Inachoka kuamini na kupenda sana mtu na mwishoe inaishia kusalitiwa na kuumizwa moyo.
Inachosha na inaumiza sana kujali, kuheshimu na kuonesha uaminifu lakini unaambulia kudanganywa na kupigwa danadana !
Inachosha kuwa na mipango mingi ya mbali na mtu ambaye lengo lake ni la muda mfupi!
Hivyo, kabla hujamjaji mtu, ukamwita majina mabaya na kumlaumu katika msimamo wake wa maisha, hebu fikiria kwanza ni nini kimemfanya awe hivyo.
Vaa viatu vyao na uone maumivu waliyopitia. Wamepitia mengi ya kuumiza na kukatisha tamaa katika mahusiano. Hofu hiyo bado imewajaa mioyoni mwao. Hawana uhakika na yupi atakayefaa kupewa tena nafasi mioyoni mwao.
Ndio, wanayo mapenzi ya dhati, lakini uhakika wa nani apewe ndio haupo. Kama mtu akikupenda, jaribu kumuelewa, jaribu kumjali, jaribu kumuonesha kwamba, wewe sio kama wale wengine.
“The best and most beautiful things in this world cannot be seen or even heard, but must be felt with the heart. Keep love in