Wamiliki wa biashara wa Afrika wanaotegemea mitandao ya kijamii kuendesha mauzo yao wanakadiria hasara waliyopata baada ya huduma za mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, na Instagram kupotea kwa saa sita.

Wataalamu wanasema huduma za biashara za kimtandao, ambazo zimepata ukuaji mkubwa barani Afrika wakati wa janga la corona ziliathiriwa vibaya.

“Walioathiriwa zaidi ni wale wanaojitegemea na wenye biashara ndogo, ikilinganishwa na wale wenye bishara kubwa ambazo zina tovuti,” Mtaalamu wa mauzo ya kidijitali Karen Wambugu aliambia BBC.

Aliongeza: “Wakati mitandao mikubwa ya kijamii kama vile Facebook na Instagram hazifanyi kazi, wenye biashara ndogo ndogo hawawezi kuendesha mauzo yao kwa sababu hawana njia nyingine mbadala.”

Mama mfanyabishara wa Ghana ambaye anaendesha biashara yake ya chakula mtandaoni na pia kuuza vyakula vyake katika hoteli iliyopo mji mkuu wa Accra anasema huduma hizo zilikatika wakati wa shughuli nyingi za chakula cha mchana.

“Asilimia 80 ya mauzo yetu hutokana na wateja wanaoagiza vyakula kupitia mtandaoni. Ni wateja wachache wanaoweza kufika hotelini wakati kuna msongamano wa magari kuja kula ” Kafui Adza aliambia BBC.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles