Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na maafa ya Uviko-19. Biashara nyingi kote duniani zimepatwa na changamoto za aina tofauti tofauti hususani kupungua kwa masoko kutokana na nchi nyingi kuweka vizuizi vya kusafiri abiria na hata usafirishaji wa bidhaa.

Akizungumza kwenye hafla ya mafunzo ya mauzo kwa wajasiliamali iliofanyika katikati ya wiki hii jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Pantrek Co. Bwana Hamphrey Peterson alisema biashara nyingi, ndogo na kubwa, zimelazimika kupunguza wafanyikazi wake na kuto kutoa nafasi mpya za ajira.

Mkurugenzi huyo alienendelea kusema pamoja na hayo ni sekta moja tu imeonyesha kuhimili vishindo vya kiuchumi vilivo sababishwa na janga hili na sekta hio ni sekta ya mauzo ya moja kwa moja.

Takwimu kutoka IMF zinaonyesha uchumi wa ulimwengu ulipungua 4.4% mwaka 2020, lakini wakati huoo huo, sekta ya mauzo ya moja kwa moja ilikua kwa takribani 2.3%

Kwa sababu hii, sekta ya mauzo ya moja kwa moja ndio sekta pekee iliongeza biashara na nafasi za ajira kwa asilimia kubwa kuliko sekta zote katika kipindi chote cha maafa ya Uviko-19. Pia, sekta hii imeonyesha kutoa ajiria zaidi kwa wanawake ambao wako tayari kua wajasiliamali.

Kwa kuwapa wanawake nafasi ya kujiajiri, sekta ya mauzo ya moja kwa moja imewawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi.

Advertisement

Akizungumza kwenye hafla hio hio, Bi. Rosemary Shadrack, spokesperson for Africa Marketing Inc. Alisema bado ni wasichana wachache wanao hitimu sekondari na vyuo vikuu ukifananisha na wavulana.

Kwa kukosa nafasi ya kusoma, watoto wakike wanakua pia na nafasi ndogo ya kuajiriwa na ndio maana kipindi cha Uviko-19 ni wanawake walio pata adha kubwa zaidi kiuchumi. Kwa vile kuanzisha biashara ya mauzo ya moja kwa moja haigarimu mtaji mkubwa, wanawake wengi wamefanikiwa kuanzisha biashara zao wenyewe hususan kwa njia ya mtandao hasa kwa kutumia simu za mkononi.

“Kufungua duka ni gharama kubwa, kuna kodi ya fremu, ulipie miezi sita mpaka mwaka na baada ya hapo kuna matengenezo labda shelfu, friji, mapambo na kadhalika hapo bado huja hesabia mtaji wakuchukua bidhaa utakazo uza hapo dukani, alafu kuna swala la kodi,” alisema Aisha Mwanakombo mjasiliamali jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hio hio, mjasiliamali huo alieleza, “…kwa kweli ni gharama kubwa kufungua duka la kawaida, lakini kwa kufanya biashara ya mauzo ya moja kwa moja, mtaji ni mdogo maana unahitaji tu fedha ndogo kuchukua bidhaa zako za mwanzo baada ya hapo unawatembezea wateja wako popote walipo badala ya kufungua duka.”

Bi. Mwanakombo alifafanua kwamba kwa dunia ya sasa ambapo matumizi ya simu za mkononi yamesambaa kote nchini, basi mauzo ya moja kwa moja ni rahisi sana.

“Na weza kuwafikia wateja kwa kuwa rushia picha kwenye magrupu na mteja akakupigia simu na kuweka oda,” aliongezea.

Swala lingine linalo wavutia wanawake wengi kwenye mauzo ya moja kwa moja ni swala zima la muda. Wanawake wengi wanamajukumu ya nyumbani aidha kulea na kadhalika, hivio kufanya biashara ya moja kwa moja kupita simu au kutembelea wateja iinampa muda wa kuwa nyumbani na wanawe au kufanya shughuli zingine ilihali anaendelea na mauzo ya moja kwa moja kwenye simu au kwa kujipangia ratiba ya kutembelea wateja wake.

Zaidi ya hapo, kuna swala la ujuzi, kama tulivo ona takwimu za uhitimu wa shule kwa upande wa wanawake ni mdogo, hivio wanawake wengi hawana ujuzi maalumu wa shuleni unao hitajika kama kigezo cha ajira au hata kufunngua biashara.

Lakini kwenye biashara ya moja kwa moja, hakuna ujuzi maalumu unaohitajika zaidi ya kujituma kutangaza biashara yako kwa wateja. Hii inafanyika kirahisi kwa njia ya simu kwenye mitandao ya kijamii au kwa kutembelea wateja majumbani, ofisini au kwenye kiusanyiko ya kirafiki au kifamilia.

Kurahisisha mambo, kampuni nyingi zinazo jihusisha na mauzo ya moja kwa moja hutoa mafunzo ya wali na mafunzo endelevu kuwsaidia wajasiliamali kuanzisha na kukuza biashara zao.

Na hizi ndio sababu kuu zinazo wavutia wanawake wengi kufanya biashara za moja kwa moja. Mpaka sasa, takwimu zinaonyesha kuwa takribani 75% ya wafanyabiashara za moja kwa moja kote duniani ni wanawake.

Kwa wasiofahamu, mauzo ya moja kwa moja ni mfumo wa biashara ambapo kamouni kubwa zinakusanya bidhaa za aina mbali mbali na kuwawezesha wajasiliamali kuanza kusambaza bidhaaa hizo. Kampuni hizi hutoa mafunzo ya mauzo kwa wajasiliamali kuwawezesha kuanzisha biashara zao.

Bidhaa zinazo uzwa kwa mfumo huu ni za kila aina zikiwemo vifaa vya nyumbani kama vile viombo na mapambo, vyakula na virutubisho, vipodozi, mafazi nk.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles