Kiongozi huyo pia amelalamikia shambulizi la anga la hivi karibuni lililoua watu kadhaa kwenye kambi ya watu waliokoseshwa makazi jimboni Tigray. Ikulu ya Marekani imesema kwamba viongozi hao wawili walizungumzia mikakati kuelekea kusitishwa kwa mapigano ambayo kwa kipindi cha takriban miezi 14 yameua maelfu ya watu huku mamilioni wakilazimika kutoroka makwao.

Ripoti zimeongeza kusema kwamba Biden alisisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa upelekaji wa misaada nchini Ethiopia pamoja na haki za binadamu kwa wale walioathiriwa na mapigano, wakati kukiwa na wasiwasi kutokana na watu waliozuiliwa baada ya hali ya dharura kutangazwa nchini humo.

Marekani hata hivyo haijatoa taarifa zozote kuhusiana na alivyosema Abiy baada ya kuzungumza na Biden. Hata hivyo viongozi hao wawili wanasemekana kuzungumzia umuhimu wa kuimarishwa kwa uhusiano kati ya Marekani na Ethiopia.

Tagged in: