AfricaSwahili News

Biden, Merkel washindwa kukubaliana kuhusu Nord Stream 2

 

Rais Joe Biden wa Marekani na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wameshindwa kumaliza tofauti zao kuhusu mradi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Urusi hadi Ulaya lakini wamekubaliana kwamba Moscow haitaruhusiwa kutumia nishati kama silaha dhidi ya mataifa jirani. 

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Washington wakati wa ziara ya Kansela Merkel nchini Marekani, viongozi hao wawili wamesema bado wanatofautiana kuhusu bomba hilo la Nord Stream 2 litakalosafirisha gesi kutoka Urusi kwenda mataifa ya Ulaya kupitia Ujerumani. 

Biden amesema ingawa baadhi ya wakati mitazamo ya washirika hutofautiana lakini amemweleza wazi wazi Kansela Merkel wasiwasi wake kuhusu mradi huo. 

Mradi huo wa dola bilioni 11 umekuwa kitovu cha msuguano kati ya Marekani na Ujerumani, huku Washington ikisema utaleta kitisho cha usalama kwa kuongeza utegemezi wa Ulaya kwa nishati ya gesi kutoka Urusi madai ambayo Ujerumani imeyapinga.

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.