Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Bilioni 4.2 kutumika kukamilisha ujenzi wa jengo la madarasa na maabara chuo cha ufundi Arusha

Advertisement Scroll To Keep Reading

 

Serikali inatarajia kutumia zaidi ya Shilingi bilioni 4.2 katika mwaka wa fedha 2021/22 kukamilisha ujenzi wa jengo la madarasa na maabara katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

Advertisement Scroll To Keep Reading

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akiwa ziarani Jijini Arusha ambapo amesema jengo hilo litakuwa na ghorofa tatu lenye maabara, madarasa, ofisi na stoo.

Amesema mpaka sasa ujenzi wa jengo hilo umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 2.6 na kwamba hadi kukamilika litatumia jumla ya Shilingi bilioni 6.8.

 “Lengo la Serikali ni kuhakikisha inaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili kuweza kuzalisha wataalamu watakaokuwa na umahiri unaohitajika katika soko la sasa la ajira,” amesisitiza Mhe. Kipanga.

Awali akitoa taarifa ya miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa chuoni hapo, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Musa Chacha amesema chuo kimepokea jumla ya Shilingi bilioni 1.499 kutoka Serikalini kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 420 likikamilika na kwamba ujenzi wake umefikia asilimia 15.

Amesema chuo pia kina mradi wa ujenzi wa kliniki itakayogharimu takribani Shilingi bilioni moja ambazo zitatokana na mapato ya ndani na kwamba ujenzi wake umefikia asilimia 30.

Aidha Dkt. Chacha amesema  chuo kupitia maabara zake kimetafiti na kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa matumizi ya jamii ikiwemo vipukuswa vyenye ubora, barakoa na dawa ya kunywa kwa waathirika wa UVIKO-19 ili kupambana na janga la ugonjwa huo.

Naibu Waziri Kipanga yupo Jijini Arusha kwa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi katika vyuo na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.