Baada ya utata wa miaka mingi, hatimaye bintimfalme wa Japan Mako ataweza kuolewa na kijana aliyesoma naye na kuwa tayari kuacha wadhfa wake wa kifalme.

Shirika la Imperial Household limesema, tarehe ya ndoa tayari imepangwa kuwa Oktoba 26.

Awali, wapenzi hao walipanga kuoana mwaka 2018, lakini ndoa yao ilisitishwa baada ya kubainika kuwa familia ya bwana Komuro ilikuwa ina matatizo ya kifedha.

Baada ya ndoa , walitarajia kuhamia Marekani , sehemu ambayo bwana Komuro anafanya kazi ya uwakili.

Hatua hiyo imeandikwa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Bintimfalme huyu alifuatiliwa sana na vyombo vya habari – wakati baba yake ndiye anashikilia taji la mwanamfalme Fumihito -.

Aidha ,familia ya bwana Komuro imemsababishia mwanamfalme kupata msongo wa mawazo kwa miaka kadhaa, shirika la Imperial Household lilisema, kwa mujibu wa chanzo cha habari cha Kyodo.

Shangazi yake, Empress Masako, pia alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa unaohusiana na msongo wa mawazo ,baada ya kupata msukumo mkubwa wa kupata mtoto wa kiume ili awe mrithi. Mara nyingi kuna unyanyapaa wa magonjwa ya akili nchini Japan.

Wapenzi hao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2012 wakiwa wanafunzi wa chuo kikuu cha International Christian mjini Tokyo.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles