Advertisement Scroll To Keep Reading
Swahili News

Boaz, Kingai kizimbani kesi ya Mbowe

Advertisement Scroll To Keep Reading

By James Magai

By Hadija Jumanne

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa Rushwa na Uhujumu Uchumi leo itaanza kupokea ushahidi wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mashahidi hao ni pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi, akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai.

Wengine ni maofisa wa Polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo vitengo vya makosa ya kimtandao, uchunguzi wa silaha na uchunguzi wa maandishi na wengine kutoka mikoani.

Mashahidi wengine ni maaskari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), akiwamo Luteni Denis Leo Urio kutoka Kikosi cha Jeshi cha Makomandoo, 92 KJ Ngerengere, mkoani Morogoro.

Soma zaidi:Mashahidi 24 vielelezo 19 kesi ya Mbowe na wenzake

Pia wamo maofisa wa sheria kutoka kampuni za huduma za simu za mkononi za Mic Tanzania Ltd (Tigo) na Airtel.

Advertisement

Soma zaidi: Ole Sabaya, IGP Sirro kuwa mashahidi kesi ya Mbowe

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa maarufu kama Adamoo na Mohamed Abdillahi Ling’wenya.

This article Belongs to

News Source link

Advertisement Scroll To Keep Reading

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.