Advertisement Scroll To Keep Reading
Swahili News

BoT yapokea maombi manane leseni maduka fedha za kigeni

Advertisement Scroll To Keep Reading

By Sharon Sauwa

Dodoma. Serikali imesema hadi kufikia Julai 30 mwaka 2021, Benki Kuu Tanzania (BoT) imepokea maombi mapya manne ya leseni ya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni ambazo yanafanyiwa uchambuzi na wahusika watapewa leseni iwapo watakidhi vigezo.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Masauni wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Mjini (CCM) Priscus Tarimo.

 “Nini hatma ya biashara ya maduka ya kubadilisha fedha nchini (Bureau de Change) yaliyofungwa na Serikali nchini kote,” ameuliza Tarimo.

Akijibu swali hilo, Masauni amesema maduka ambayo hayakufungwa yameendelea kufungua matawi na kutoa huduma hizo katika miji mbalimbali nchini.

Soma zaidi:Gambo: Ulikuwa uporaji shughuli ya kufunga maduka ya kubadilisha fedha za kigeni

Amesema kwa ujumla, hali ya upatikanaji wa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni nchini Tanzania ni ya kuridhisha.

Advertisement

Aidha Masauni amesema maduka yaliyofungwa pamoja na makampuni mengi yanayotaka kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni nchini, yanaruhusiwa kuomba leseni Benki Kuu.

Amesema waombaji wanatakiwa kuzingatia matakwa ya sheria za fedha za kigeni ya mwaka 1992 na kanuni za biashara ya kubadilisha fedha za kigeni ya mwaka 2019.

Soma zaidi:Mbunge ataka wafanyabiashara maduka ya kubadilisha fedha kurejeshewa fedha zao

Amesema hadi kufikia Julai 30 mwaka 2021, Benki Kuu ilikua imepokea maombi mapya manne ya leseni ya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni ambazo yanafanyiwa uchambuzi na wahusika watapewa leseni iwapo watakuwa wamekidhi vigezo.

This article Belongs to

News Source link

Advertisement Scroll To Keep Reading

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.