AfricaSwahili News

CCM Kilimanjaro yasema chanjo ya corona iwe hiari na siyo lazima

Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Kilimanjaro kimewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona na kueleza kuwa mpango wa chanjo ya ugonjwa huo utakuwa wa hiari na siyo lazima.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi ameyasema hayo leo Julai 20, 2021 wakati akizungumza na wananchi wa kada mbalimbali waliofika katika ofisi za chama hicho mkoani humo.

Boisafi amesema Serikali imeingia kwenye mpango wa chanjo kitaifa na demokrasia ni mpango huo wa chanjo kuwa jambo la hiari na siyo la lazima.

Amewataka Watanzania kutambua kuwa ugonjwa wa corona upo pamoja na magonjwa mengine, hivyo waendelee kuchukua tahadhari kwa kila hatua na kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya, ikiwemo kunawa mikono kwa  sabuni na maji tiririka, kuepuka misongamano na kuvaa barakoa.

“Hatutawalazimisha wala kuwashurutisha, wananchi kuchanjwa, kama hawataki huo ndio mpango wetu na tunaendelea kusema tufuate masharti na ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya, juu ya kuchukua tahadhari za corona,”

“Kinachotusikitisha sana, vyama vya upinzani, vimekuja na utaratibu wao, tena wanataka kuilazimisha Serikali kwamba kuchanjwa ni lazima, sisi kama CCM, kama wenye serikali, hatutakuwa tayari, kuchanja watu kwa lazima, tutachanja watu kwa hiari yao.”

“Na hao wa upinzani, kama kweli wanajua maana ya demokrasia, maana yake mtu anatakiwa awe na uhuru wa kujiamulia mambo yake, kama wanataka serikali ya CCM ilazimishe, sisi tunawapelekea salamu, hatutamlazimisha Mtanzania kufanyiwa chanjo, ataamua mwenyewe.”

 

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.