More
  - Advertisement -

  Chad yataja serikali mpya ya mpito

  -

  - Ad Keep reading below -

  Utawala wa kijeshi uliochukua mamlaka mwezi uliopita nchini Chad kufuatia kifo cha rais Idriss Deby Itno umekamilisha kuunda serikali mpya ya mpito. 

  Kulingana na msemaji wa jeshi Azem Bermandoa, Baraza la Kijeshi la Mpito (CMT) linaloongoza kwa sasa limeahidi kurejesha demokrasia katika kipindi cha miezi 18 baada ya kile ambacho upinzani ulikitaja kama mapinduzi ya kitaasisi.

  - Ad Keep reading below -

  Bermandoa amesema kupitia hotuba ya televisheni kwamba rais Mahamat Deby mtoto wa rais Deby ameitangaza serikali hiyo yenye mawaziri 40 pamoja na manaibu na kuunda wizara ya maridhiano ya kitaifa itakayoongozwa na Acheick ibn Oumar aliyekuwa kiongozi wa waasi, ambaye mwaka 2019 alichaguliwa mshauri wa rais wa masuala ya diplomasia.

  Mpinzani mwingine mwandamizi Mahamat Ahmat Alhabo ataongoza wizara ya sheria. Wengi wa mawaziri kwenye serikali hii ya mpito hata hivyo wanatokea kwenye serikali iliyopita.

  - Ad Keep reading below -

  Kiongozi wa upinzani Success Masra ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba hii haitawafikisha kokote iwapo hawatarejea kwenye misingi inayozingatia matakwa ya wananchi, ambayo ni kuwa na rais wa kiraia, na makamu kutoka jeshi. Amesema uteuzi huo unatoa taswira ya ujenzi wa nyumba unaoanzia kwenye paa.

  ALSO READ  VIDEO: Naibu Waziri Aweso awasweka ndani wasimamizi bodi ya maji
  ALSO READ  Sijaridhishwa na gawio linalotolewa na Kiwanda cha Kilombero - Waziri Mkuu

  Chad imejikuta katika mzozo baada ya kifo cha Idriss Deby kilichotangazwa siku moja tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Aprili 11 ambapo alikuwa aongoze kwa muhula wa sita.

  Jeshi limesema watu sita wamekufa wiki iliyopita kufuatia maandamano ya kuupinga utawala wa kijeshi katika mji mkuu N’Djamena na eneo la kusini, ingawa wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema ni watu tisa.

  Kwenye maziko ya wahanga hao yaliyofanyika siku ya Jumamosi, mwanaharakati wa haki za binaadamu Serge Ngardji alipomzungumzia mwandamanaji Djigolem Yannick, aliyeuawa kwenye maandamano hayo alisema wataendelea kupigania haki zao katika kuhakikisha kizazi kijacho kinakuwa na maisha bora.

  - Ad Keep reading below -

  Amesema “Tutaendeleza mapambano, tutaendeleza ili kujitoa kwetu kusiwe kazi bure. Lazima tuendelee kupambana ili maisha ya kesho ya ndugu zetu yawe mazuri. Lazima tuendelee kupambana ili kesho ya ndugu zake wawe na maisha mazuri ama hata wapate fursa ya kwenda shule na kutibiwa. Kwa hivyo tutaendelea ili kuwe na uhuru.”

  ALSO READ  Oparanya Praised for Oxygen Project in Kakamega [VIDEO]

  Zaidi ya watu 650 wanashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia maandamano hayo yaliyozuiwa na mamlaka. Aidha, hapo jana jeshi liliondoa kizuizi cha kutotoka nje usiku kilichotangazwa baada ya kifo cha rais Deby.

  ALSO READ  Jeshi kuongoza Mali kwa muda

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Shocking Leicester display raises serious questions about ability to handle pressure

  Leicester's top-four hoodoo returned as they collapsed in the 4-2 loss to Newcastle United.

  Postpone LG election to avoid another legal gymnastics – ex-Oyo Gov, Alao-Akala tells Makinde

  A former Governor of Oyo State, Chief Christopher Adebayo Alao-Akala, has advised the incumbent Governor, Engineer Seyi Makinde, to without wasting more time, postpone...

  FBI hails EFCC for efforts on global crime war

  The Federal Bureau of Investigation (FBI) considers the Economic and Financial Crimes Commission (EFCC) a critical partner in the global fight against organized crime...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -
  %d bloggers like this: