Rais wa Chile Sebastian Pinera ametangaza hali ya dharura katika jamii 72 zinazoishi kusini mwa taifa hilo, wakati kukishuhudiwa ghasia na mashambulizi ambayo mara nyingine yanadaiwa kufanywa na makundi ya watu wa asili ya Mapuche. 

 
Makundi hayo yanashinikiza kurejeshwa kwa ardhi za wazee wao. Amri hiyo ya rais inahusisha ukomo wa uhuru wa kukusanyika na kutembea pamoja na kuruhusu wanajeshi kuwasaidia polisi. 
 
 Amri kama hiyo ya rais inaweza kutekelezwa kwa hadi siku 15 na kuanzishwa upya kwa siku 15 nyingine, iwapo bunge litaridhia. 
 
Hatua hiyo imeathiri jamii 40 katika jimbo la Biobio na 32 za La Araucania. Rais Pinera amesema hali hiyo ya dharura inalenga kuilinda jamii, kurejesha usalama wa umma na utawala wa sheria.