Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Cristiano Ronaldo: Sijakuja Manchester United kwa likizo

Advertisement Scroll To Keep Reading


Cristiano Ronaldo anasema hajarejea Manchester United “kwa likizo ” huku kapteni huyo wa Ureno akijiandaa kwa ajili ya kurejea nyumbani katika uwanja wa Old Trafford Jumamosi.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Katika mkataba wake wa kwanza na Mashetani wekundu , Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 alifunga mabao 118 katika mechi 292 katika kipindi cha miaka sita ya mafanikio katika klabu hiyo ya Kaskazini Magharibi.

“Nina uwezo,” Ronaldo aliuambia wavuti rasmi wa Manchester United. “Niko tayari kuanza.”

Wenyeji wa United ni Newcastle katika Ligi ya premia katika mechi itakayong’oa nanga saa tisa alasiri kwa saa za Uingereza sawa na saa kumi na moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki

Kusainiwa upya kwa mkataba wa Ronaldo na Manchester United wenye thamani ya pauni milioni 12.8 kutoka Juventus ilikuwa habari kubwa zaidi ya uhamisho msimu huu kwani mahasimu wa Manchester United, Manchester City walionekana kuwa ndio wangemchukua mshambuliaji huyo.

Nyota huyo wa Ureno, ambaye atavaa jezi namba saba kwa mara nyingine tena, alishinda mataji mawili ya Ligi ya Primia , ligi ya klabu bingwa Ulaya mara moja, Vikombe viwili vya Ligi , Kombe moja la FA-pamoja , Kombe la Fifa la Dunia pamoja na lile la Community Shield – chini ya meneja wa zamani Sir Alex Ferguson.

Ingawa Manchester United wameshinda mataji tangu Ronaldo aondoke kuelekea timu kubwa ya Uhispania ya Real Madrid mwaka 2009, hawajaweza kupata taji la juu tangu msimu wa soka wa 2012-13

“Ndio maana niko hapa,” alisema. “Siko hapa kwa ajili ya likizo.

“Awali nilifanikiwa kushinda vitu muhimu, na nilivaa fulana sawa na hii , miaka mingi iliyopita, lakini niko hapa kushinda tena.

Je kuwasili kwa Ronaldo kutakuwa msukumo wa mazuri au uwepo wake na hadhi yake vitawakera wachezaji wenzake kikosini?

Wakati alipofunga mabao ya dakika za mwisho yaliyoifanya Ureno kufuzu kwa Kombe la dunia dhidi ya Jamuhuri ya Ireland kwa kichwa wiki iliyopita, alikuwa amekosa mikwaju ya penati aliyoichukua kabla ya Bruno Fernandes, ambaye ana rekodi bora ya mikwaju ya aina hii katika United.

Solskjaer anahitaji kusimamia vyema kikosi cha wachezaji kama meneja wakati huu ambapo United inafuatiliwa kwa karibu.

Mechi ya Newcastle inapaswa kuwa sherehe. Mara ya mwisho Ronaldo alipocheza dhidi yao katika Old Trafford, alishinda mabao matatu kwa mpigo katika ushindi wa 6-0.

Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba hakuna mahali pa kujificha kwa wachezaji wake tangu kuwasili kwa Cristiano Ronaldo.

Kuwasili kwake na kule kwa beki wa Ufaransa Raphael Varane , kumeongeza matarajio ya timu hiyo , katika klabu ambayo mara ya mwisho kushinda taji la ligi ilikuwa 2013.

Solskjaer alisema : “Ataingia uwanjani wakati mmoja kwa kweli.”

Raia huyo wa Norway aliongezea: Hakuna mahali pa kujificha kwa washindi kama hawa. Huwezi kujitolea asilimia 95 katika mazoezi na ushindwe kuonesha umahiri wako. Hivyo ndivyo anavyojitolea yeye mwenyewe hivyobasi anahitaji wengine wajitolee kama yeye.

”Ndio kiwango cha mahitaji ya Ronaldo ambacho alikuwa nacho 2008 wakati wa mwisho akiichezea Man United dhidi ya Newcastle alipofunga ‘hatrick na kuisaidia timu yake kuwalaza wageni hao 6-0”.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.