Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Nickson Simon amewataka watu kuutazama Mkoa wa Pwani kwa ukubwa zaidi kwani ndio Dar es Salaam ijayo.

Mh. Nickson akiapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe

Mh. Nickson ameeleza kwamba kutokana na kuwa Jiji la Dar es salaam limeshajaa hivyo maendeleo na fursa nyingi za kiuwekezaji zitafanyika kwenye Mkoa unaokua kwa kasi ambao ni  Pwani.

Ameongeza kwamba maendeleo ya Miundombinu kwa Mkoa wa Pwani yanaendelea kufanyika ukiwa ni pamoja na Mwendokasi, na kuongeza kwamba fursa ya kilimo, madini nk.

“Pwani ni next Dar es salaam, watu wa Dar inabidi mlijue hili. Fursa zilizopo Pwani nazo tunataka ziwanufaishe watu wetu ndiyo maana tunataka kuwajengea uwezo watu wetu, huu ni mpango wa  Mkoa wa Pwani.  Tunawakaribisha wawekezaji wa Makazi, Kilimo na fursa zingine nyingi,” Nickson

Tagged in:

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles