AfricaSwahili News

DC Karatu aridhishwa na hatua za ujenzi wa miradi ya Elimu na Afya

 

Maabara ya somo la biolojia katika shule ya sekondari ya Diego imekamilika na imeanza kutumika kwa wanafunzi kuanza kujifunza kusoma kwa njia ya vitendo somo la Biolojia. Kukamilika kwa maabara hiyo kutasaidia wanafunzi zaidi ya mia mbili na hamsini wa masomo ya sayansi.

Hayo yamebainika katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati alipotembelea shule ya sekondari ya Diego iliyopo kata ya Rhotia kujionea ujenzi wa miundombinu ya elimu. 

Ujenzi wa maabara hiyo umegharimu kiasi cha million 47 mpaka kukamilika kwake, nguvu za wananchi ikiwa ni shilingi Million 15 na serikali million 32. 

Katika ziara hiyo Mh. Kayanda amekagua ujenzi wa matundu kumi ya choo yaliyojengwa kwa gharama ya million 18 wananchi wakiwa wamechangia million 10 na serikali wamechangia million 8.Mh. Kayanda ameelekeza kamati ya ujenzi katika sekondari ya Diego kurekebisha dosari ndogo zilizojitokeza katika ukamilishaji wa ujenzi ili kuweka miundombinu hiyo katika ubora.

Katika ziara hiyo Mh. Kayanda alitembelea na kujionea ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari ya Kilimatembo. 

Ujenzi huo ni matundu 10 ya vyoo vya wanawake na matundu 10 ya vyoo vya wavulana. Katika ziara hiyo ameelekeza ujenzi kuwa umekamilika mpaka kufikia tarehe ishirini na tano mwezi wa saba mwaka huu.

Wakati huo huo Mh. Kayanda ametembelea zahanati ya huduma iliyopo katika kijiji cha huduma na kujionea jengo la kichomea taka ambalo limekamilika katika ujenzi wake. 

Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea na kuangalia miundombinu ya ujenzi wa zahanati, iliyopewa shilingi million 50 kukamilisha ujenzi wake. Mh. Kayanda ameelekeza kwa uongozi wa kijiji na kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo kusimamia ujenzi mpaka kufikia tarehe kumi na tano mwezi wa nane mwaka huu.

Katika majumuisho ya ziara hiyo Mh. Kayanda amesema ameridhishwa na hatua za ujenzi wa miradi hiyo ya elimu na afya. Amesema ni vyema viongozi wakazingatia thamani ya ujenzi miradi inaendana kiasi cha fedha zilizotolewa. 

Wakati huo huo Mh. Kayanda amewaambia viongozi wa serikali za vijiji na watendaji wa serikali kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa virusi vya covid-19. Kwa kuelimisha wananchi kunawa kwa maji tiririka na vitakasa mikono.

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.