AfricaSwahili News

DC Njombe acharuka mradi wa shule ulioibiwa vifaa

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa ameiagiza TAKUKURU na Jeshi la Polisi kuchunguza na kuwakamata watu wote waliohusika na wizi wa vifaa vya ujenzi wa shule shikizi ya msingi ya Mji Mwema hatua ambayo imekwamisha kuendelea na shughuli za ujenzi wa shule hiyo.

Ujenzi wa shule hiyo ambao umeanza kwa michango ya wananchi na kisha serikali na wadau kuchangia kiasi cha fedha na vifaa vya ujenzi ulioanza mwanzoni mwa mwaka huu umekuwa ukiharakishwa kwa lengo la kukomesha changamoto mrundikano wa watoto zaidi ya 200 katika vyumba vya madarasa vya shule kongwe ya Mji Mwema yenye wanafunzi wanaopindukia 1500.

Ujenzi wa mradi huo uliibuliwa na wananchi wa kata ya Mji Mwema ambapo kupitia mkutano wa hadhara wakakubaliana  kuchangishana fedha kiasi cha elfu 20 kwa kila kichwa huku familia zenye wazazi wawili zikipaswa kuchangia elfu 40 jambo ambalo lilifanikiwa ila watu wasio waaminifu wakaingia tamaa na kuanza kuiba vifaa vya ujenzi zikiwemo Bati,saruji na noto jambo linalomuibua mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa na kulazimika kutoa kauli.

Akiweka bayana hatua alizochukua hadi sasa ili kunusuru mradi huo Diwani wa kata ya Mji Mwema Nestory Mahenge anasema amemtafuta fundi aliehusika na wizi huo na kurejesha vitu vyotr huku akisema katika mradi huo kumekuwa na vikwazo vingi vya kisiasa kutoka kwa wagombea wenza wa ndani na nje cha chama chake.

Kwa upande wao wananchi akiwemo Neema Sanga na Alfa Pembe wasema wamechukizwa na kitendo mafundi kwa kushirikiana na watu wasiowatakia mema watoto wao kuiba vifaa vya ujenzi ili kukwamisha mradi huo ambao umefika hatua nzuri kwa nguvu za wananchi na kuitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika wote wa wizi.

Shule ya Msingi Mji mwema inatajwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ikiwa na wanafunzi takribani 1500 huku darasa moja likiwa na watoto wasiopungua 200.

 

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.