Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha ASP Sunday Ibrahim, amemzuia dereva wa basi la Arusha Express, linalofanya safari kati ya Arusha na Mbeya kuendelea na safari hii leo na kuagiza atafutwe dereva mwingine baada ya yeye kukiuka sheria za usalama.

Hayo yamejiri hii leo Oktoba Mosi, 2021, wakati Kaimu Mkuu huyo alipoongozana na wakaguzi wa magari kufanya ukaguzi na kutoa elimu kwa madereva na abiria kutumia vyombo hivyo kwa kuzingatia sheria na kuepusha ajali za barabarani.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles