Staa wa Bongo  Diamond  ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho. Mkali huyo ametumia kiasi cha $25K ambazo ni zaidi ya milioni 57 kwa pesa ya Kitanzania kununua saa mpya aina ya Rolex. Kwa mujibu wa risiti ya ununuzi wa saa hiyo.

Diamond Platnumz ambaye kwasasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake ya kimuziki, alitembelea duka maarufu la Watch Empire huko Los Angeles na kujipatia saa hiyo yenye warantii ya miaka miwili.

Diamond anaungana na mastaa kama Davido, Drake, Jay Z, Kanye West n.k ambao hupendelea kuvaa saa za aina ya Rolex.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles