By Jesse Mikofu

Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ametuma  salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha Jaji wa Mahakam Kuu ya Zanzibar, Haji Omar Haji.

Kifo cha Jaji Haji kimetokea leo Jumamosi Septemba 11, 2021 katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar na anatarajiwa kuzikwa kesho Shakani, Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Katika salamu hizo za rambirambi, Dk Mwinyi amesema amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Jaji Haji Omar Haji.

“Mwenyezi Mungu ampe rehema na kumjaalia makazi mema peponi. Amin,”

Marehemu Jaji Haji aliteuliwa na Rais Mwinyi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Februari Mosi, 2021 na kuapishwa Februari 8.

Pia, Agosti 16, 2021 Jaji Haji Omar aliteuliwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Jaji Omar Othman Makungu kuwa Jaji Mkaazi Pemba.

Advertisement

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles