Advertisement Scroll To Keep Reading
Swahili News

Dkt Stergomena L Tax mwanamke wa kwanza kuteuliwa waziri wa Ulinzi Tanzania

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dkt. Tax ni mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kushika wadhifa katika Wizara ya Ulinzi. Hivi karibuni alimaliza muda wake akihudumu kama katibu mtendaji katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na pia amewahi kuwa katibu mkuu katika wizara mbali mbali nchini Tanzania, katika wizara za Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Viwanda, Biashara na Masoko na Fedha na Mipango.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Rais Samia pia amemteua Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Faustine Ndugulile ambaye ameondolewa katika wadhifa huo.

January Yusuf Makamba ambaye aliwahi kushika wadhifa wa uwaziri na naibu waziri, ameteuliwa kuwa Waziri wa Nishati ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Medard Matogolo Kalemani ambaye naye pia amefutwa kazi na rais.

Rais pia amemteua Prof. Makame Mnyaa Mbarawa kuwa waziri wa Ujenzi na Uchukuzi. Dkt. Leonard Madaraka Chamuhiro ambaye alikuwa akishikilia wadhifa naye amefutwa kazi.

Dkt. Aliezer Mbuki Feleshi, ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo anachukua nafasi inayoachwa wazi wa Prof. Adelardus Kilango ambaye ameteuliwa kuwa balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Feleshi alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.