in ,

DR Congo yatangaza kutokomezwa kwa mlipuko wa Ebola

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kutokomezwa kwa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa wa Ebola uliosababisha vifo vya watu sita.

Tangazo hilo linakuja miezi mitatu baada ya ugonjwa huo kuripotiwa kuibuka tena huko Kivu Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la Afya Dunia (WHO) limeangazia tangazo hilo katika Twitter yake Jumatatu.

Muda mfupi uliopita DRC ilipongezwa na Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dr. Matshidiso Moeti

Katika taarifa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef limesema hatua ya haraka iliyochukuliwa na serikali na washirika wake ilisaidia kudhibiti mlipuko.

Lilisema kuwa huo ulikuwa mlipuko wa tatu wa Ebola kukumba nchi hiyo chini ya mwaka mmoja.

Kabla ya kuanza kwa mlipuko huo Februarui 7, nchi hiyo ilikuwa imetangaza kumalizika kwa ule wa 11 uliosababisha vifo vya wati 55 kati ya visa 130 vya maambukizi vilivyothibitishwa kwa karibu miezi sita.

DR YEGERA NI BINGWA NA MTAFITI WA TIBA ASILI ALIYEJALIWA KUWA NA HOFU YA MUNGU

Coastal wakanusha, kumfuta kazi kocha Mgunda