Msemaji wa serikali Billene Seyoum amesema kwamba shambulizi la leo la angani, limelenga kituo cha mafunzo kinachotumika na wapiganaji wa Tigray.

Amesema kuwa kituo hicho kimekuwa kikitumika kama kituvo cha shughuli za kundi hilo la wapiganaji.

Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, imekuwa ikipigana na kundi la Tigray TPLF kwa mda wa mwaka mmoja sasa, japo kundi hilo halijakuwa likitekeleza mashambulizi makali tangu mwezi Juni, serikali ilipotwaa sehemu kubwa za kaskazini mwa Ethiopia.

Idadi kubwa ya wanajeshi wa serikali wameondoka sehemu hiyo.

Jeshi la angani la Ethiopia lilianza mashambulio kutoka angani siku ya jumatatu kwa kulenga mji wa Mekele, mji mkuu wa jimbo ya Tigray.

Umoja wa mataifa umesema kwamba shambulizi hilo liliua Watoto watatu na kujeruhi watu kadhaa, na kutoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano hayo.

Tagged in: