Ethiopia imesema inawafukuza maofisa saba wa juu wa Umoja wa Mataifa kwa kuingilia masuala ya ndani.

Ujumbe wa Tweeter kutoka wizara ya mambo ya nje imesema maofisa hao wana saa 72 kuondoka nchini humo.

Hivi karibuni UN imetoa wasiwasi wake kuhusu suala la kuweka vizuizi vya kutoruhusu misaada kuingia Tigray kwa kipindi cha miezi mitatu.

Mkuu wa misaada ya Umoja wa Mataifa Martin Griffiths alisema mapema wiki hii kuwa anadhani eneo hilo linakabiliwa na njaa kwa sasa.

Na kuitaka serikali kurusu maroli yaweze kupita , aliliambia shirika la habari la Reuters: “Huu ni mpango uliopangwa na serikali inaweza kurekebisha sheria hizo.”

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles