Halmshauri Kuu ya Umoja wa Ulaya inatazamiwa hii leo kutoa mapendekezo yake kuhusu suluhisho la mzozo na Uingereza juu ya Ireland ya Kaskazini. 

Makamu wa rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya na mjumbe wa Brexit Maros Sefcovic anatarajiwa kuwasilisha mipango ya umoja huo kuhusu namna ya kupunguza ugumu wa kufanya biashara uliosababishwa na kile kinachoitwa itifaki ya Ireland Kaskazini. 

Hii huenda ikajumuisha kutoa nafuu kwa baadhi ya bidhaa kama vile vyakula fulani na dawa. Chini ya itifaki hiyo, Ireland Kaskazini inaendelea kufuata sheria za soko moja na forodha za Umoja wa Ulaya, na hivyo kuzuwia ukaguzi wa mpakani kati ya jimbo hilo la Uingereza na Jamhuri ya Ireland, ambayo ni mwanacham wa Umoja wa Ulaya. 

Siku ya Jumanne, waziri wa Brexit wa Uingereza David Frost, alitoa wito wa kuifanyiwa mabadiliko kamili itifaki hiyo, akisisitiza miongoni mwa mambo mengine, kusitishwa kwa jukumu la mahakama ya sheria ya Ulaya kusimamia itifaki hiyo.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles