Usikubali mtu akukatishe tamaa kuwa huwezi kufanya jambo fulani. Kama umelifanyia utafiti ukaona linawezekana, umejipanga kulifanya na unaona kabisa ndilo unalotaka kulifanya, lifanye. Usisikilize watu wanaokukatisha tamaa. Wengi wetu huangalia yale ambayo hatuwezi kuyafanya, au tumetamani kuyafanya ila tunaogopa na kuwakatisha tamaa wale wanaojaribu kulifanya. Wanaokatisha tamaa hufanya hivyo kuogopa kuwa utafanikiwa na wao wameshindwa au wanaogopa kujaribu.

Miaka kadhaa iliyopita nilikiwa nataka kufanya jambo fulani na kweli nilijua kabisa nitafanikiwa, nilipoomba ushauri kwa niliowaona wanajua zaidi kuhusu mambo hayo walinikatisha tamaa sana kwa kwa sababu nilikuwa sijajiamimi nikaacha, ila niliumia sana moyo na hasa pale alipokuja kulifanya mwingine maana ilikuwa ni opportunity ya kufaa sana. Sasa nimejifunza na hakika naona ambavyo mtu unaweza kufika mbali sana kama utaweka nguvu zako zote kufanyia kazi ndoto zako na kutosikiliza wanaokatisha tamaa.

Fanya utafiti wa kutosha, Fanya kazi kwa bidii, Usikate tamaa na hakika kufanikiwa ni lazima.

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles