By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Akiyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye amechukua fomu kuwania kiti cha Uspika.
Ole-Medeye aliyekuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Kilimo kati ya mwaka 2010 hadi 2015 amechukua fomu hiyo leo Jumanne Januari 11, 2022 katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini hapa.

Hatua hiyo inakuja baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Job Ngugai kujiuzulu Januari 6 mwaka huu.

Soma hapa: Msukuma achukua fomu kumrithi Job Ndugai
Ole Medeye ambaye anakuwa mtu wa pili leo kujitokeza katika ofisi hizo kuchukia fomu, akitanguliwa na Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma ambaye pia amechukua fomu kuwania nafasi hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa Ole Medeye kugombea nafasi hiyo kwani alishaahi kujitokeza tena mwaka 2015 akiwa Chadema, lakini hakufanikiwa.

Soma hapa: Tisa wachukua fomu CCM kugombea uspika

Akizungumza mara baada ya kutoka kuchukua fomu hiyo, Ole Medeye amesema kilichomsukuma kukitaka kiti hicho ni katika kuimarisha Bunge.

Advertisement

“Kama mnavyojua dola ina mihimili mitatu ambayo ni Serikali, Mahakama na Bunge,kila kimoja kinatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi,hivyo mimi kama nitakuwa  Spika nitaweza kuimarisha mhimilili huo katika uongozi wangu,” amesema Ole-Medeye.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles