Advertisement Scroll To Keep Reading
Michezo (Swahili)Swahili News

Hans Poppe afariki dunia – Mwanaspoti

Advertisement Scroll To Keep Reading

By Khatimu Naheka

Advertisement Scroll To Keep Reading

Taarifa mbaya kwa medani ya michezo ni kwamba aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba Zakaria Hans Poppe amefariki dunia.

Hans Poppe amefikwa na umauti usiku huu katika Hospitali ya Aga Khan alikokuwa amepumzishwa kwa zaidi ya wiki mbili.

Klabu ya Simba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram umethibitisha taarifa hizo za kifo cha kiongozi huyo ambaye amewahi kushikilia nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya wekundu hao kwa kipindi kirefu.

Inaelezwa kwamba hali ya Hans Poppe ilibadilika ghafla ndani ya siku tatu na kumpelekea kufariki leo usiku.

Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Simba Salim Abdallah ‘Try Again amesema siku tatu nyuma HansPope alikuwa anaendelea vyema kiasi cha kuchat katika makundi mbalimbali ya WhatsApp hali ambayo iliwapa imani kwamba wakati wowote ataruhusiwa kutoka hospitali.

“Hali yake ilibadilika ghafla ndani ya siku tatu kutoka leo lakini kabla ya hapo bodi nzima tulijua kwamba angeruhusiwa alikuwa akijadiliana mambo mbalimbali kwenye makundi yetu ya WhatsApp, hili la usiku huu sio tu limetushtua ila limetuumiza sana,” amesema Try again

Advertisement

Hans Poppe atakumbukwa kwa misimamo yake mikali ndani na nje ya Simba lakini pia  kuwa mstari wa mbele kuipigania Simba kwa fedha na mambo mbalimbali hatua ambayo ilimjengea heshima kubwaNews Source link

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.