Kocha wa Golden State Warriors, Steven Kerr amethibitisha kuwa nyota wake Andrew Wiggins amepata chanjo ya Covid-19 na nyota huyo yupo tayari kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa NBA unaotaraji kuaza Oktoba 19, 2021.

Kerr amethibitisha hilo usiku wa kuamkia leo Oktoba 4, 2021 wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari ju ya maandalizi ya timu yake kuelekea msimu mpya wa NBA.

Taarifa hiyo imekuwa gumzo kwasababu Andrew Waggins alisema hapo awali kuwa hayupo tayari kuchanja kutokana na sababu za kiimani na kugusia atafikiria kufanya hivyo kama atalazimishwa na mamlaka husika.

Kuelekea msimu mpya wa NBA, wasimamizi wa ligi hiyo waliweka wazi kuwa wachezaji, benchi la ufundi na wahusika wote wanapaswa wapate chanjo ya Covid-19 huku ikiripotiwa 90% ya wachezaji wamepata chanjo.

Kama Andrew Wiggins asingechanja basi asinge ruhusiwa kucheza michezo yote ya Golden State Warriors ambayo ingechezwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kwenye mji wa St. Francisco.

Mchezaji nyota ambaye haijulikani kama amepata chanjo au laa ni Kyrie Irving wa Brooklyn Nets ambaye awali hakuchanja na haonekani kwenye mikusanyiko ya pamoja na timu yake kwenye maandalizi kuelekea msimu mpya.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles