Shirika la Fedha Duniani(IMF) limesema kuwa haliwezi kukisia kukua kwa kiwango cha Pato ndani la Ethiopia kwa kipindi cha mwaka 2022-2026 kufuatia kile wanachosema kuwa ni “kiwango cha juu cha kutokuwa na uhakika”.

Hali inakuja kufuatia mzozo uliochukua miezi kumi na moja katika eneo la kaskazini la Tigray.

IMF imetoa makadirio ya uchumi ya dunia kwa kukadiria kukua kwa pato la ndani kwa nchi kuwa 2% kwa mwaka 2021, ambayo iko chini kwa 6% ya mwaka 2020.

Kwa kulinganisha, na nchi jirani ya Eritrea- ambayo pia inahusika katika mzozo huo – itaona ukuaji wa 4.8% kwa 2022-2026.

Kenya- ambayo ina uchumi mkubwa Afrika Mashariki- kwa upande mwingine, utaongezeka kwa 6% katika kipindi hicho hicho.

Katika muongo mmoja uliopita, Ethiopia ilikuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi, kwa kuongezeka hata mara mbili ya takwimu ya kiwango kilichopita.

Hata hivyo uchumi wake umeathirika kutokana na ukame, mvutano ya kikabila wakati huohuo wataalam pia wameonya juu ya kulipwa kwa deni lake la kigeni ambalo lilifadhili miradi mikubwa ya miundombinu.

Nchi zingine ambazo IMF haikutoa makadirio ni Afghanistan, Libya na Syria- na nchi zote zilizokumbwa na mizozo.

Ripoti ya IMF ilisema uchumi wa duniani unakadiriwa kukua asilimia 5.9 mnamo 2021 na asilimia 4.9 mnamo 2022, asilimia 0.1 chini kwa 2021 kuliko makadirio ya Julai.

Mlipuko wa janga la corona pia umeathiri uchumi haswa wa nchi zinazoendelea.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles