Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Iran yaruhusu wakaguzi wa kimataifa katika vituo vyake vya nyuklia

Advertisement Scroll To Keep Reading

Iran imekubali leo Jumapili kuwaruhusu wakaguzi wa kimataifa kuweka vifaa vya ufuatiliaji katika vituo vyake vya nyuklia na kuendelea kuchukua vidio na kukusanya taarifa juu ya shughuli zake. 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Tangazo hilo limetolewa na Mohammad Eslami ambaye anaongoza shirika la nishati ya Atomiki la Iran baada ya kufanya mkutano na Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia IAEA Rafael Grossi mjini Tehran. 

Tangazo hilo huenda likaipa muda zaidi Iran kuelekea kwa mkutano wa bodi ya IAEA wiki hii ambapo mataifa yenye nguvu duniani yameikosoa Iran kwa kutoonyesha ushirikiano na wakaguzi wa kimataifa.

Tehran imezuia taarifa zake zote juu ya oparasheni kwenye vituo vyake vya nyuklia wakati mazungumzo juu ya kuunusuru mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 ya mjini Vienna yamekwama.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.