Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Jeshi la Guinea lataka benki kufungia akaunti zote za serikali

Advertisement Scroll To Keep Reading


Mamlaka ya kijeshi ya Guinea, junta imeamuru benki kufungia akaunti zote zinazohusiana na serikali ili “kupata mali za serikali”.

Junta, ambayo ilichukua udhibiti wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, inasema agizo hilo linaathiri akaunti za taasisi na watu binafsi wa serikali inayomaliza muda wake.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Maofisa wa juu wa serikali ya Rais aliyeondolewa madarakani Alpha Condé hawataweza kutumia akaunti zao.

Viongozi wa mapinduzi walichukua madaraka Jumapili, na walisema wanataka kumaliza ufisadi uliokithiri, ukiukwaji wa haki za binadamu na usimamizi mbaya.

Guinean authorities.Jumuiya ya eneo la Magharibi mwa Afrika Ecowas – ambayo inataka katiba kufatwa – imetuma ujumbe wa kutaka kufanya mazungumzo na mamlaka ya Guinea.

Jumuiya hiyo imetaka Rais Condé ambaye ameshikiliwa na jeshi kuachiwa huru.

 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.