Na Maridhia Ngemela, mwanza.

Wananchi wamemlilia Mkuu wa Wilaya juu ya gharama kubwa ya umeme ambao imekuwa kero sugu kwa wananchi na kusababisha kukosa huduma hiyo inavyotakiwa.

Wakazi wa Wilaya ya Ilemela kata ya Kayenze kisiwa cha Bezi  Mkoani Mwanza wamemwambia mkuu wa Wilaya hiyo Hassan Masala alipotembelea kisiwani hapo kwa lengo la kukagua  miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi ndipo alipokutana na kero ya umeme kwa wananchi hao walioamua kuelezea malalamiko yao juu ya kampuni isiyo ya kiserikali ya Power Gen inayosambaza umeme kisiwani hapo na kusababisha ukosefu wa huduma hiyo kama Serikali inavyotaka.

Miongoni mwa wananchi waliozungumza kwa niaba ya wengine wamesema kuwa, umeme ni njia moja wapo ya kuleta maendeleo na Mkuu wa Wilaya hii kampuni ya Power Gen ni kama ya wizi maana walitubadirishia mfumo na kila siku inatakiwa ulipie shilingi elfu 1000 ya umeme yaani huu umeme umekuwa kama unanunua vocha tunakuomba mkuu wa Wilaya mtubadirishie kampuni itakayotuwezesha kupata umeme wa uhakika,na mkuu tunaomba tupate muda sahihi wa kufika kwa kivuko maana muda haujulikani na kinapofika usiku hatujui kimebeba watu wa namna gani tunaomba uzungumze na Mkurugenzi apange muda sahihi wa kufika kwa kivuko wamesema wananchi wa kisiwa cha Bezi.

Naye Mkuu wa Wilaya Hassan Masala alipokuwa akiwajibu wananchi juu ya kero ambazo wamemueleza amesema,napata changamoto kujibu maswali kwasababu muhusika hayupo tunatambua kuwa anatoa huduma kwa wananchi wetu tunachotaka sisi ni kuwajengea wao uwezo wa shughuli ambazo sisi tunapaswa kufanya juu ya utoaji huduma na hapa lazima tanesco mfahamu  kuwa kunachangamoto  wananchi hawa wanataka umeme na kwavile hapa muhusika mkuu hayupo mimi  niombee tumuandikie barua ya wito ili tuje tuzungumze nae tuone mikataba yake inasemaje ili tuone tutatoa msaada gani maana angelikuwepo hapa angetoa majibu na kuwaelimisha wananchi na hii ziara siyo ya kushutukiza sasa anakimbia Kimbia ili iweje kwahiyo hili nalichukua nitalifanyia kazi kwa haraka zaidi amesema Masala.

Aidh Masala amewakumbusha wazazi kujiandaa kwaajili ya maandalizi ya kuwapeleka watoto shule  ili kuondoka mimba za utotoni na kutowafanyisha biashara bali wapatiwe elimu maana Serikali inawekeza huko ili watoto waweze kupata elimu.

“Moja ya changamoto niliyoiyona hapa katika kisiwa hiki ambayo ni  hatarishi ni mimba za utotoni kwahiyo swala la uhamasishaji wa mimba kwa watoto wetu ni kutoa elimu na tutaita viongozi wetu tuwape maelekezo namna ya kufanya na nimeona watoto wengine wako mitaani sina uhakika kama wote  wanasoma kutokana na umbali na moja ya kipaumbele ni kujenga Shule ya sekondari ndani ya kisiwa hiki ili kuondoa watoto katika kusafiri umbali wa mwendo mrefu  kwa kufuata kivuko kwenda shule na tuna mikakati ya kujenga mabweni ili kutokomeza mimba za utotoni amesema Masala.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles