AfricaSwahili News

JKT yawaita vijana wengine kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria mwaka 2021

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Rajab Mabele ameongeza majina ya Vijana waliohitimu elimu ya kidato cha Sita mwaka 2021 kwenda kuungana na vijana wenzao walioitwa hapo awali kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria katika kambi walizopangiwa mara moja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 10,2021 kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la kujenga taifa Brigedia Jenerali Rajabu Mabele, Kaimu Mkuu wa utawala JKT Kanali Hassan Mabena,amesema kuwa mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu tu.

“Naomba kusisitiza hapa,mafunzo ya vijana hawa kwa mwaka huu ni miezi mitatu tu na siyo mwaka mmoja kama ambavyo inasemekana hivi sasa,huko mitaani kuna watu wanasema mafunzo ni mwaka mmoja,hii siyo kweli” amesema Kanali Mabena

“Maneno hayo yamesababisha baadhi ya vijana kukata tamaa ya kuhudhuria mafunzo,kimsingi upo mpango wa kuongeza muda hadi kufikia mwaka mmoja lakini suala hill bado lipo kwenye majadiliano,na hivyo kwa mwaka huu mafunzo ni miezi mitatu kama kawaida.”

Amesema kuwa vijana walioitwa awali na bado hawajaripoti pamoja na walioitwa awamu hii ya pili ,wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa mara moja ambapo mwisho kuripoti ni Juni 17 mwaka huu.

Pia  Kanali Mabena amesema kuwa ,wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia makundi hayo.

“Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote walioitwa kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo,umoja wa Kitaifa,stadi za kazi,stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa,”amesema Kanali Mabena.

Kanali Mabena amesema kuwa orodha kamili ya majina ya vijana walioitwa ,Makambi ya JKT waliyopangiwa na meneo yaliyopo pamoja na vifaa vinvyotakiwa kwenda navyo ,inapatikana katika tovuti ya JKT www.JKT.go.tz.

 

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.