Advertisement Scroll To Keep Reading
Swahili News

Kamati maalum kuchunguza kutoweka kwa jasusi, kubuniwa Somalia

Advertisement Scroll To Keep Reading

Idara ya NISA mapema mwezi huu ilisema kwamba Bi Ikran Tahlil Farah alitoweka Juni na kwamba alitekwa nyara na kuuwawa na wanamgambo wa al- Shabab. Hata hivyo al- Shabab wamekanusha madai hayo wakati mama wa jasusi huyo Qali Mohamud Guhad akiilaumu NISA kutokana na kifo kinachodaiwa kutokea.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Guhad ameikataa kamati ya uchunguzi ya rais ambayo itajumuisha mwakakilishi kutoka NISA. Guhad wakati akiongea na Muhabarishaji Idhaa ya kisomali alisema kwamba kiongozi wa nchi hajasema lolote kwa zaidi ya miezi mitatu tangu kutoweka kwa mwanawe.

Ameongeza kusema kwamba ana imani na mahakama ya kijeshi inayoendelea kufanya uchunguzi kuhusu kutoweka kwa Farah. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Abdimalik Abdullahi amesema kwamba ni jeshi pekee linaloweza kufanya uchunguzi wa kina kwa kuwa taasisi nyingine za serikali haziaminiki.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.